Digital resources in the Social Sciences and Humanities OpenEdition Our platforms OpenEdition Books OpenEdition Journals Hypotheses Calenda Libraries OpenEdition Freemium Follow us

Team Members / Wajumbe wa Timu

Listed in alphabetical order /
Washiriki wameorodheshwa kwa mpangilio wa alfabeti.

Prof. Dr. Bettina Brockmeyer

My name is Bettina Brockmeyer. I am a Professor of Modern History at Justus Liebig University Giessen and the responsible coordinator of MRIC in Germany. I am enthusiastic about the fundamentally collaborative nature of the project and hope that it will be able to achieve its many important goals. Jina langu ni Bettina Brockmeyer. Mimi ni Profesa wa Historia ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Justus Liebig mjini Giessen na ni mratibu mkuu wa mradi wa MRIC nchini Ujerumani. Nimehamasishwa sana na asili ya ushirikiano wa karibu ambayo ndiyo msingi wa mradi huu, na nina matumaini kwamba utaweza kufanikisha malengo yake mengi muhimu.

Hellen Robert Gabriel

My name is Hellen Robert Gabriel and I am 5th generation descendant of Mangi Ngalami of Siha, one of the Chagga chiefs who was executed by the German colonial administration in 1900 in the Kilimanjaro Region of Tanzania. This family connection gives me a personal link to the history that our project seeks to research, document, and share. In the project, I serve as the contact person and support the coordination of research and exhibition activities.
I am particularly looking forward to 2 major outcomes

1)I am especially hoping that through this project we may be able to contribute to locating and identifying his remains, and to clarifying further historical details, including accounts that he may have been executed alongside his brother, whose identity and story remain unclear. I look forward to the project helping to uncover these missing pieces of history and to bringing greater recognition and understanding of this period.

⁠2) Contributing to a better understanding of this important chapter of Tanzanian history and ensuring that the stories of those who resisted colonial rule are remembered. I hope the project will help foster dialogue, historical awareness, and recognition of the lasting impact of colonial violence on local communities.

Jina langu ni Hellen Robert Gabriel. Mimi mzao wa kizazi cha tano cha Mangi Ngalami wa Siha, mmoja wa machifu wa Chagga ambaye aliuawa na utawala wa kikoloni wa Ujerumani mnamo mwaka 1900 katika Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania. Uhusiano huu wa kifamilia unanipa muunganiko wa karibu na historia ambayo mradi wetu unakusudia kuitafiti, kuihifadhi katika maandishi na kuisambaza kwa wengine. Katika mradi huu, ninahudumu kama afisa wa mawasiliano na ninasaidia uratibu wa shughuli za utafiti na maonesho.
Ninatazamia kwa hamu matokeo mawili muhimu ya mradi huu.

1) Ninatumaini sana kwamba kupitia mradi huu tutaweza kuchangia katika juhudi za kutafuta na kutambua masalia yake, pamoja na kufafanua kwa undani zaidi taarifa za kihistoria zinazohusiana naye. Hii ni pamoja na madai kwamba huenda aliuawa pamoja na kaka yake, ambaye utambulisho wake na historia yake bado havijaeleweka kikamilifu. Ninatazamia mradi huu kusaidia kufichua vipande hivi vya historia vilivyopotea na kuchangia katika kuongeza utambuzi na uelewa mkubwa wa kipindi hiki muhimu cha kihistoria.


⁠2) Kuchangia katika kuimarisha uelewa wa sura hii muhimu ya historia ya Tanzania na kuhakikisha kwamba simulizi za wale waliopinga utawala wa kikoloni zinakumbukwa na kuhifadhiwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Ninatumaini kwamba mradi huu utachangia katika kukuza majadiliano yenye tija, kuimarisha uelewa wa historia, na kuongeza utambuzi kuhusu athari za kudumu za ukatili wa kikoloni kwa jamii za wenyeji.

My name is Lena Guth, I am a Student Assistant at Justus Liebig University Giessen. As such, my work in the project is mostly administrative. I am looking forward not only to expand my own knowledge but also to make the information the researchers uncover accessible for everyone. Jina langu ni Lena Guth, mimi ni mwanafunzi msaidizi katika Chuo Kikuu cha Justus Liebig mjini Giessen nchini Ujerumani. Kwa hivyo, kazi yangu katika mradi huu ni ya kiutawala zaidi. Ninatarajia siyo tu kupanua maarifa yangu mwenyewe bali pia kufanya matokeo na taarifa ambazo watafiti wanazipata zipatikane, zifikike na kueleweka kwa kila mtu.

Ulrike Kirsch

My name is Ulrike Kirsch. I earned an M.A. in African Studies in Leipzig and Dar es Salaam, with a focus on Tanzanian regional studies. I completed my postdoctoral fellowship (2021–2023) at the Ethnological Museum Berlin, where I conducted research and curatorial work on the history of German-Tanzanian colonial ties. As a research assistant at the MRIC at Justus Liebig University Giessen, I focus in particular on belongings. I hope that the MRIC will lay the groundwork for future repatriations and restitutions of ancestors and belongings to northern Tanzania. I also hope that the project will contribute to the public discourse in Germany regarding colonial injustices and their lasting effects. Jina langu ni Ulrike Kirsch. Nilipata Shahada ya Uzamili (M.A.) katika Masomo ya Afrika huko Leipzig na Dar es Salaam, nikijikita katika tafiti za maeneo mbalimbali ya Tanzania. Nilikamilisha masomo yangu wa baada ya shahada ya uzamivu (Postdoctoral Fellowship) kati ya mwaka (2021 – 2023) katika Jumba la Makumbusho la Ethnolojia ya Berlin, ambapo nilifanya utafiti na kazi ya uangalizi kuhusu historia ya uhusiano wa kikoloni kati ya Ujerumani na Tanzania. Kama Msaidizi wa Utafiti katika mradi wa MRIC katika Chuo Kikuu cha Justus Liebig Giessen, ninajikita hasa katika utafiti wa mali na vitu vya urithi wa kitamaduni. INatumai kwamba mradi wa MRIC itaweka msingi wa kurejeshwa kwa mababu na mali zao kaskazini mwa Tanzania katika siku zijazo. Pia natumai kwamba mradi huo utachangia katika mjadala wa umma nchini Ujerumani kuhusu dhuluma za kikoloni na athari zake za kudumu.

Konradin Kunze

I am Konradin Kunze, an artistic (provenance) researcher as well as a theatre and exhibition maker. I studied acting and worked at various theatres in Germany. With Flinn Works, I develop transnational theatre projects and exhibitions. I also work on the identification of abducted ancestral remains and belongings, supporting Tanzanian descendant families in their demands for repatriation. I was the artistic director of the research exhibition Marejesho and am involved in the research projects ProHumStra at Université de Strasbourg and AnceStra at EHESS Paris. I live with my family in Berlin.


Together with Isabelle Reimann and Valence Silayo, I initiated the Marejesho Research and Information Centre project at Justus Liebig University Giessen and Better Nation Foundation. My role in the project is artistic provenance researcher. I am responsible for installing and updating the Marejesho exhibition in Moshi. I also contribute to the research overall and help connect the two sub-projects.

Mimi ni Konradin Kunze, mtafiti wa kisanaa wa historia ya asili na umiliki wa makusanyo (provenance researcher), pamoja na mbunifu wa maonyesho ya jukwaani (theatre) na maonesho ya makumbusho na sanaa (exhibitions). Nilisomea uigizaji na nimefanya kazi katika kumbi mbalimbali za sanaa za maonyesho nchini Ujerumani. Kwa kutumia Flinn Works, ninaendeleza miradi na maonyesho ya kimataifa. Pia ninafanya kazi katika utambuzi wa masalia ya mababu waliotekwa nyara na mali zao, pia ninasaidia familia za wazao wa mababu hao wa Tanzania katika madai yao ya kurejeshwa nyumbani kwa masalia ya binadamu na mali kale. Nilikuwa Mkurugenzi wa Kisanaa wa maonesho ya utafiti ya Marejesho na ninashiriki katika miradi ya utafiti ya ProHumStra katika Chuo Kikuu cha Strasbourg na AnceStra katika EHESS Paris. Ninaishi Berlin pamoja na familia yangu.


Pamoja na Isabelle Reimann na Valence Silayo, nilianzisha mradi wa Marejesho Research and Information Centre katika Chuo Kikuu cha Justus Liebig Giessen na Better Nation Foundation. Jukumu langu katika mradi huu ni kuwa mtafiti wa kisanaa wa historia ya asili na umiliki wa makusanyo (artistic provenance researcher). Ninawajibika kwa kusimika na kusasisha maonesho ya Marejesho mjini Moshi. Pia ninachangia katika shughuli za utafiti kwa ujumla na kusaidia kuunganisha sehemu mbili za mradi huu.

Mnyaka Sururu Mboro

My name is Mnyaka Sururu Mboro. I am a teacher and activist, and for over 40 years I have been campaigning in Germany for the repatriation of ancestral remains to Africa, and particularly to Tanzania. I am a co-founder of Berlin Postkolonial e.V. and part of the Marejesho exhibition in 2022. I act as an consultant on this project and assist with translations. My hope is that the Tanzanian and German government will find a solution to repatriate the ancestral remians soo. I wonder how many years the descendants should still wait. Jina langu ni Mnyaka Sururu Mboro. Mimi ni mwalimu na mwanaharakati. Kwa zaidi ya miaka 40 nimekuwa nikifanya kampeni nchini Ujerumani kwa ajili ya kurejeshwa kwa mabaki ya mababu barani Afrika, na hasa Tanzania. Mimi ni mwanzilishi mwenza wa asasi ya Berlin Postcolonial. na ni sehemu ya maonyesho ya Marejesho mwaka wa 2022. Ninafanya kazi kama mshauri katika mradi huu na kusaidia katika tafsiri. Matumaini yangu ni kwamba serikali ya Tanzania na Ujerumani zitapata suluhisho la kuwarejesha mabaki ya mababu hivi karibuni. Je, ni miaka mingapi zaidi ambayo wazao wa mabubu hao wanapaswa kuendelea kusubiri?

Hans Robert Mmari

I am Hans Robert Mmari, Founder and Executive Director of Better Nation Foundation, established in 2013. My role in the MRIC project is to ensure legal compliance, secure necessary permits, and support effective collaboration between our team and the researchers. I hope this project will generate meaningful knowledge, strengthen partnerships, and deliver lasting positive impact to the community. Mimi ni Hans Robert Mmari, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Better Nation Foundation, taasisi iliyoanzishwa mwaka 2013. Katika mradi wa Marejesho Research and Information Centre (MRIC), jukumu langu ni kuhakikisha uzingatiaji wa sheria na taratibu zote zinazohitajika, kupata vibali muhimu, na kusaidia kujenga ushirikiano mzuri na wenye tija kati ya timu yetu na watafiti wanaoshiriki katika mradi huu. Nina matumaini kwamba mradi huu utazalisha maarifa yenye manufaa, utaimarisha ushirikiano kati ya wadau mbalimbali, na kuleta mchango chanya wa kudumu kwa jamii.


Dr. Laibor Kalanga Moko

I am Laibor Kalanga Moko, an anthropologist and postdoctoral researcher at the Institute of Social and Cultural Anthropology at the University of Hamburg. As part of the Marejesho Research and Information Centre project team, I collaborate with Waarusha and Meru communities to investigate the provenance of their ancestral human remains and cultural belongings currently held in museums in Germany. Through this work, I seek to bring grassroots voices and perspectives into transnational debates on decolonisation and restitution. Mimi ni Laibor Kalanga Moko, mwanaanthropolojia na mtafiti wa baada ya shahada ya uzamivu (Postdoctoral Researcher) katika Taasisi ya Anthropolojia ya Jamii na Utamaduni ya Chuo Kikuu cha Hamburg. Kama sehemu ya timu ya mradi wa Marejesho Research and Information Centre, ninafanya kazi kwa ushirikiano na jamii za Waarusha na Wameru kuchunguza historia ya asili na umiliki wa masalia ya mababu zao pamoja na mali zao za kitamaduni ambazo kwa sasa zinahifadhiwa katika majumba ya makumbusho mbalimbali nchini Ujerumani. Kupitia kazi hii, ninatafuta kuleta sauti na mitazamo ya watu wa kawaida katika mijadala ya kimataifa kuhusu kuondoa ukoloni (decolonisation) na marejesho (restitution), ili kuhakikisha kwamba maoni na maslahi ya jamii zinazohusika yanawakilishwa na kusikika ipasavyo katika mijadala hiyo.

Dr. Irene Ndossi

I’m Irene Ndossi and a researcher at the Marejesho Research and Information Centre in Tanzania, where I work on provenance research that explores the histories, movements, and meanings of cultural heritage. I’m motivated by the chance to work with communities and partner institutions to uncover and document overlooked stories. I hope this project will support lasting collaborations, strengthen community engagement with cultural heritage, and contribute to more sustainable and inclusive approaches to preserving and sharing historical knowledge. Mimi ni Irene Ndossi, mtafiti katika mradi wa Marejesho Research and Information Centre nchini Tanzania, ambapo ninajihusisha na utafiti wa historia ya asili na umiliki wa makusanyo (provenance research) unaochunguza historia, safari na maana ya urithi wa kitamaduni. Ninapata motisha kupitia nafasi ya kufanya kazi kwa karibu na jamii Pamoja na taasisi washirika ili kufichua na kuandika na kuhifadhi simulizi na historia ambazo mara nyingi zimepuuzwa au kusahaulika. Nina matumaini kwamba mradi huu utasaidia kujenga ushirikiano wa kudumu, kuimarisha ushiriki wa jamii katika masuala ya urithi wa kitamaduni, na kuchangia katika kuendeleza mbinu endelevu na shirikishi zaidi za kuhifadhi, kutunza na kusambaza maarifa ya kihistoria kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Dorothea G Ndossy-Parsalaw

I am Dorothea Ndossy-Parsalaw, a PhD researcher based in Dar es Salaam-Tanzania. As a Research Assistant in the Marejesho Research and Information Centre, I contribute to provenance research that explores the histories and movements of cultural heritage. I look forward to supporting collaboration between communities and partner institutions and helping to make cultural heritage more accessible and meaningful for future generations. Mimi ni Dorothea Ndossy-Parsalaw, mtafiti wa shahada ya uzamivu (PhD) mwenye makazi yake Dar es Salaam, Tanzania. Kama Msaidizi wa Utafiti katika mradi wa Marejesho Research and Information Centre, ninachangia katika utafiti wa historia ya asili na umiliki wa makusanyo (provenance research), unaochunguza historia na harakati za urithi wa kitamaduni. Ninatarajia kusaidia kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na taasisi washirika, pamoja na kuchangia katika kufanya urithi wa kitamaduni upatikane kwa urahisi zaidi, ueleweke vizuri zaidi na uwe na maana kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Hadija Bitesha Ramadhani

My name is Hadija Bitesha Ramadhani, and my background is in compliance, project management, and business development. In the Marejesho Research and Information Centre, I am involved in the community outreach initiatives that will help connect the project with the communities it serves.
What I appreciate most about this project is its potential to create awareness about restitution and help bridge the gap between colonial history and present day understanding. I look forward to contributing to community engagement, and positive impact through the work we are doing.
Jina langu ni Hadija Bitesha Ramadhani, na taaluma yangu imejikita katika masuala ya uzingatiaji wa kanuni na taratibu (compliance), usimamizi wa miradi na maendeleo ya biashara. Katika mradi wa Marejesho Research and Information Centre, ninashiriki kwenye shughuli za uhamasishaji na mawasiliano ya jamii ambazo zitasaidia kuunganisha mradi huu na jamii zinazohudumiwa na mradi.
Kitu ninachokithamini zaidi kuhusu mradi huu ni uwezo wake wa kujenga uelewa kuhusu marejesho (restitution) na kusaidia kuziba pengo lililopo kati ya historia ya ukoloni na uelewa wa kizazi cha sasa. Ninatarajia kuchangia katika ushirikishwaji wa jamii, kujenga mahusiano mazuri na kuleta matokeo chanya kupitia kazi tunayoifanya.

Isabelle Reimann

My name is Isabelle Reimann and I work part-time as a project lead at the Marejesho Research and Information Centre in the Kilimanjaro and Arusha regions of Tanzania. Alongside this role, I work as a provenance researcher at the Institute of Anatomy at Leipzig University. I studied ethnology, psychology, and sociology and am a PhD candidate at Humboldt University of Berlin. My research focuses on the rehumanisation of human remains from colonial contexts and the critical examination of historical race research.

As an anthropologist, I wish to take responsibility for the past misconduct within my discipline, which remains unresolved to this day. I co-initiated the MRI Centre to make information locally accessible and to support community-driven provenance research in the region of origin. I hope that it will evolve into a vibrant, open and collaborative space.

Jina langu ni Isabelle Reimann na ninafanya kazi kwa muda kama Kiongozi wa Mradi katika mradi wa Marejesho Research and Information Centre katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha nchini Tanzania. Sambamba na jukumu hili, ninafanya kazi kama mtafiti wa asili na historia ya umiliki wa makusanyo (provenance researcher) katika Taasisi ya Anatomia ya Chuo Kikuu cha Leipzig. Nilisomea Ethnolojia, Saikolojia na Sosholojia, na kwa sasa ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Humboldt Berlin. Utafiti wangu unajikita katika kurejesha utu na hadhi ya masalia ya binadamu yaliyokusanywa katika mazingira ya ukoloni, pamoja na kuchunguza kwa kina na kwa mtazamo wa ukosoaji historia ya tafiti za kisayansi za ubaguzi wa rangi (race research).

Kama mwanaanthropolojia, ninatamani kuwajibika kwa makosa yaliyofanywa na taaluma yangu hapo awali, ambayo hadi leo bado hayajapatiwa ufumbuzi wa kuridhisha. Nilishiriki kuanzisha mradi wa Marejesho Research and Information Centre (MRI Centre) kwa lengo la kufanya taarifa zipatikane kwa urahisi katika jamii za wenyeji na kusaidia utafiti wa historia ya asili na umiliki wa makusanyo (provenance research) unaoongozwa na jamii husika. Natumaini kuwa kituo hiki kitaendelea kukua na kuwa mahali hai, pa wazi na pa ushirikiano, panapowaleta pamoja watu mbalimbali katika kutafuta maarifa, ukweli na haki ya kihistoria.

Emmanuel Sanare

My name is Emmanuel Sanare Lukumay, a Degree Graduate from St. Augustine University of Tanzania in Education for History and Linguistic .
I serve as Assistant Researcher for Arusha Region in this Project. I’m looking forward to contributing to meaningful research and, by the end of the Project, writing a book that captures the lessons and stories from Arusha region for future learning.
Jina langu ni Emmanuel Sanare Lukumay. Mimi ni mhitimu wa Shahada kutoka Chuo Kikuu cha St. Augustine nchini Tanzania (SAUT), nikiwa nimehitimu katika fani ya Elimu, Historia na Isimu.
Katika mradi huu, ninahudumu kama Msaidizi wa Utafiti wa Mkoa wa Arusha. Ninatarajia kuchangia katika utafiti wenye manufaa na, ifikapo mwisho wa mradi huu, kuandika kitabu kitakachohifadhi mafunzo, uzoefu na simulizi kutoka Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kujifunza kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Dr. Valence Silayo

 


My name is Valence Valerian Silayo, and I am a Lecturer in the Department of Archaeology and Heritage Studies at the University of Dar es Salaam, Tanzania. My scholarly work focuses on African archaeology, with particular attention to precolonial defence systems, socio‑political organisation, social complexity, and the material culture of precolonial societies. I also engage in research on the restitution and reparation of human remains, ethnographic collections, and community‑centred heritage management.

Alongside my academic duties, I serve as the Tanzania Project Lead for the Marejesho Research and Information Centre (MRIC), overseeing activities in the Kilimanjaro and Arusha regions. In this role, I am responsible for guiding research coordination, ensuring ethical and community‑centred engagement, and fostering productive collaboration between local communities, partner institutions, and the wider project team. I look forward to a successful project that delivers rigorous, community‑informed documentation, producing high‑quality analytical and interpretive reports, and contributing to the development of sustainable frameworks for heritage restitution and the management of ethnographic and ancestral materials.

Jina langu ni Valence Valerian Silayo. Mimi ni Mhadhiri katika Idara ya Akiolojia na Turathi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Kazi yangu ya kitaaluma inajikita katika uakiolojia wa Afrika, hususan mifumo ya ulinzi ya kabla ya ukoloni, mipangilio ya kijamii na kisiasa, miundo ya kijamii, pamoja na utamaduni wa vifaa vya kijamii. Pia ninajihusisha na utafiti kuhusu urejeshaji na fidia ya mabaki ya binadamu, mikusanyo ya kiethnografia, na usimamizi wa urithi unaozingatia sauti ya jamii miliki.

Pamoja na majukumu yangu ya kitaaluma, ninahudumu kama kiongozi wa Mradi katika Kituo cha Utafiti na Taarifa cha Marejesho (MRIC) kwa upande wa Tanzania , nikisimamia shughuli katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Katika nafasi hii, ninawajibika kuongoza uratibu wa utafiti, kuhakikisha ushirikishwaji wa kimaadili na unaozingatia jamii, na kuendeleza ushirikiano wenye tija kati ya jamii za wenyeji, taasisi washirika, na timu pana ya mradi. Natarajia utekelezaji wenye mafanikio wa mradi huu, utakaotoa taarifa za kina zinazoongozwa na Mawazo ya jamii miliki, kuandaa ripoti za uchambuzi na tafsiri zenye ubora wa juu, na kuchangia katika uundaji wa mifumo endelevu ya urejeshaji wa urithi na usimamizi wa nyenzo za kiethnografia na mabaki ya mabab

Evans Temi

I am Evans Temi, also known as Khalid. I am the son of Janet Mmari, who was the great-granddaughter of Mangi Ngalami Mmari of Siha. My role in this project is that of consultant, as I serve as the official family historian and archivist.
I look forward to helping locate his remains, honoring his legacy, and prioritizing truth-telling, even when that truth is uncomfortable. I am also looking forward to seeing who this project truly centers, and whether it remains faithful to the people, history, and legacy it claims to represent.
Mimi ni Evans Temi, pia ninafahamika kwa jina la Khalid. Mimi ni mtoto wa Bibi Janet Mmari, ambaye alikuwa kitukuu wa Mangi Ngalami Mmari wa Siha. Katika mradi huu, nina jukumu la kuwa mshauri, kwani mimi ndiye mwanahistoria rasmi wa familia na mhifadhi wa kumbukumbu za familia.
Natarajia kusaidia katika juhudi za kutafuta masalia yake, kuuenzi na kuudumisha urithi wake, pamoja na kutanguliza ukweli daima, hata pale ambapo ukweli huo unaweza kuwa mchungu au usio wa kufurahisha. Pia ninayo shauku ya kuona ni nani anayekuwa kitovu cha mradi huu, na kama utaendelea kuwa mwaminifu kwa watu, historia na urithi ambao mradi huu unadai kuuwakilisha

Highness Urio

I am Highness Urio, working as Accounts and Administration for Better Nation Foundation in the Marejesho Research and Information Centre, supporting financial management and administrative coordination. I look forward to contributing to transparent reporting and smooth operations that will help the project achieve its goals. Mimi ni Highness Urio, ninafanya kazi kama Mhasibu na Msimamizi wa Utawala katika taasisi ya Better Nation Foundation kwenye mradi wa Marejesho Research and Information Centre. Ninasaidia usimamizi wa fedha na uratibu wa shughuli za kiutawala. Natarajia kuchangia katika kuhakikisha uwazi wa taarifa za kifedha na uendeshaji mzuri wa shughuli mbalimbali ili kusaidia mradi kufikia malengo yake.