Digital resources in the Social Sciences and Humanities OpenEdition Our platforms OpenEdition Books OpenEdition Journals Hypotheses Calenda Libraries OpenEdition Freemium Follow us

Events / Matukio

July 13, 2026 /
13 Julai 2026

Community workshop (only invited guests) /
Warsha ya Jamii. Kwa wageni walioalikwa pekee

5:30: Public film screening at the Centre in Moshi /
Saa 11:30 jioni: Onesho la filamu kwa umma katika Kituo cha Marejesho, Moshi

The Empty Grave

Two families in Tanzania embark on an emotional journey to reclaim their ancestors’ human remains from German museums. A film about lost loved ones, resilience and the complexities of institutional power.

Familia mbili nchini Tanzania zinaanza safari ya kihisia ya kudai kurejeshwa kwa mabaki ya miili ya mababu zao kutoka katika makumbusho ya Ujerumani. Hii ni filamu kuhusu wapendwa waliopotea, ustahimilivu, na ugumu wa mamlaka ya taasisi.

Directors: Agnes Lisa Wegner, Cece Mlay
Production: kurhaus production and Kijiweni Productions in co-production with ZDF – Das kleine Fernsehspiel

https://www.kijiweniproductions.com/films/the-empty-grave

July 11, 2026/
11 Julai 2026

8:30 Official opening of the Marejesho Research and Information Centre (only invited guests) /Ufunguzi rasmi wa Kituo cha Utafiti na Taarifa cha Marejesho. Kwa wageni walioalikwa pekee.

„Meet the team“ /
Kutana na timu

From 10 am onwards: The public is welcome to visit the exhibition and meet the team. Welcome! /
Kuanzia saa 4:00 asubuhi na kuendelea: Umma unakaribishwa kutembelea maonesho na kukutana na timu. Karibuni!

4 pm: Public film screening /
Saa 10:00 jioni: Onesho la filamu kwa umma

4pm: Public film screening /
Saa 10:00 jioni: Onesho la filamu kwa umma.

The Empty Grave

Two families in Tanzania embark on an emotional journey to reclaim their ancestors’ human remains from German museums. A film about lost loved ones, resilience and the complexities of institutional power.

Familia mbili nchini Tanzania zinaanza safari ya kihisia ya kudai kurejeshwa kwa mabaki ya miili ya mababu zao kutoka katika makumbusho ya Ujerumani. Hii ni filamu kuhusu wapendwa waliopotea, ustahimilivu, na ugumu wa mamlaka ya taasisi.

Directors: Agnes Lisa Wegner, Cece Mlay
Production: kurhaus production and Kijiweni Productions in co-production with ZDF – Das kleine Fernsehspiel

https://www.kijiweniproductions.com/films/the-empty-grave

Pre-premiere screening: Kilichobaki – What Remains

Bagamoyo Film Collective

Kilichobaki – What Remains follows communities in Northern Tanzania as they engage with a history that is often archived elsewhere. Through encounters with photographs of looted objects, stories passed down through generations, and discussions sparked by the traveling research exhibition Marajesho, the film explores how colonial violence continues to affect families, identities, and demands for restitution today. Rather than treating history as distant, the film shows how it is lived, remembered, and negotiated in the present.

Kilichobaki – What Remains inafuatilia jamii za Kaskazini mwa Tanzania zinavyokabiliana na historia ambayo mara nyingi huhifadhiwa kwingineko. Kupitia mikutano na picha za vitu vilivyoporwa, simulizi zilizorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi, na majadiliano yaliyochochewa na maonesho ya utafiti yanayosafiri ya Marejesho, filamu hii inachunguza jinsi ukatili wa kikoloni unavyoendelea kuathiri familia, utambulisho, na madai ya urejeshaji hadi leo.

Badala ya kuichukulia historia kama jambo la mbali, filamu hii inaonesha jinsi historia hiyo inavyoendelea kuishi, kukumbukwa, na kujadiliwa katika maisha ya sasa.

July 10, 2026/
10 Julai 2026

We are sorry. The Opening had to be postponed to July 11. Thank you for your understanding.

Samahani, tarehe ya ufunguzi KDC imesogezwa mbele kutokana na sababu sizozuilika zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Ufunguzi rasmi utafanyika tarehe 11.7.2026 siku ya jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi (8:30 am). Asante sana kwa ushirikiano wenu.

June 26, 2026